Monday 31 October 2011

Tatizo langu la Kiswahili

Tarehe 31, Mwezi wa Kumi

Niliwasili uamuzi wangu wa kuandika blog hii kutokana na hamu yangu ya kuendeleza uwezo wangu wa kuwasiliana kwa lugha hiyo ya Kiswahili. Asaa blog hiyo itafika kwenye internet, upande mwingine pengine nitaona aibu mno kwa sababu ya lugha yangu na sitapata nguvu ya kutosha kutoka kwa moyoni mwangu ili nichapishe kazi hiyo katika mazingira ya hadhara.

Kuhusu jambo la Kiswahili change nimekuta tatizo mmoka kuu. Ninaweza kuwaelewa watu wanapoongea lakini kwa minajili ya haya yangu sipendi kuchangia katika mazungumzo.

Kwa hivyo nina ombi moja wasomaji wapendwa. Nawaombeni, kama ukikuta na ukisoma blog hiyo, tafadhali mrekebishe makosa katika sarufi na misamiati yangu. Pia, mjisikie uhuru kunisaidia kuongezea msamiati wangu kwa kunipatia nahau, misemo na methali. Mkifanya hivyo sina shaka kwamba nitafaulu katika Kiswahili changu!

Asanteni sana.